Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 17, 2015

BOSSOU NA KAMUSOKO WAMPA JEURI PLUIJM

BOSSOU  (KULIA) AKIMDHIBITI DIDIER DROGBA.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amewaangalia wachezaji wapya wa kikosi hicho na kutamka kuwa bado wanaendelea kusoma mazingira, akasisitiza kuwa, wanabadilika taratibu na wakizoea mazingira kwa asilimia mia, watakuwa moto na kuwezesha kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo amefunguka hayo, baada ya kuulizwa juu ya wachezaji wake wake wa kigeni katika kikosi hicho. Yanga imesajili Wazimbabwe wawili, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ‘Ras’ na beki kutoka Togo, Vincent Bossou.                                                       
Kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana, alisema wachezaji wake wa kimataifa tayari wameanza kuwa fiti, lakini wakizoea mazingira ya Bongo watakuwa katika kiwango kikubwa zaidi na kuwa msaada mkubwa kwa klabu yake inayojiandaa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Siwezi kumchambua mchezaji mmojammoja lakini kama hawa wachezaji wa kimataifa wapya wakirekebisha yale makosa machache na wakaelewa vyema, basi watakuwa na msaada katika timu mbeleni,” alisema Pluijm.

Ikumbukwe kuwa, Yanga ipo katika maandalizi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, Agosti 22, mwaka huu.       

No comments:

Post a Comment