Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 4, 2015

VITO FC YA LINDI KUANZA MASHINDANO YA VIJANA FINLAND



WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Helsinki Cup 2015, timu ya FC Vito Kilwa kutoka Kilwa mkoani Lindi,kesho wataanza harakati za kuwania ubingwa wa michuano hiyo, inayoanza kesho na kumalizika Julai 10, jijini Helsinki nchini Finland.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na waratibu wa michuano hiyo, FC Vito Kilwa wanakata utepe saa 8 mchana kwa saa za Finland dhidi ya na FC Reipas ya Oranssi, kwenye Uwanja wa 9A Käpylä, kabla ya Jumatatu kucheza na Halikko United uwanjani hapo. 

Katika mechi ya tatu kwenye michuano hiyo, jioni ya kesho Jumatatu FC Vito Kilwa watashuka tena kwenye dimba la 9B Käpylä, ambako watachuana na NJS ya Keltainen, kisha Jumanne asubuhi itawavaa Euran Pallo kwenye Uwanja wa 15B Lauttasaari.

 FC Vito ambao wako mashindanoni wakiwa na kikosi cha wachezaji 12, watashuka tena dimbani Jumanne saa 5 asubuhi kukipiga na HJK ya Kannelmäki Sininen, mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa 15A Lauttasaari. 

Akizungumzia ratiba hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Sports Development Aid (SDA), ambayo inaimiliki FC Vito kwa ushirikiano na Liike Finland ya Finland, Chigogolo Mohamed, alisema wameipokea kwa mikono miwili na wako fiti kuikabili. 

Wachezaji wa FC Vito iliyoagwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, ni Charles Fulco, Hussein Bandari, Hussein Hassani, Shabani Mpogolo, Rashidi Masimba na Hassani Salum. 

Wengine ni Yahaya Ruambo, Alex Muhando, Shabani Kikali, Twahir Ismail, Arafat Babu na Ahmad Kokolo, ambao wako chini ya kocha Mohamed Mtule na Mkuu wa Msafara (H.O.D), ni Chigogolo.

 Helsinki Cup ni michuano ya nne kwa ukubwa miongoni mwa mashindano ya vijana barani Ulaya na mwaka huu inashirikisha zaidi ya timu 1,200,  ambayo itafikia tamati Julai 10 kwenye viwanja mbalimbali jijini Helsinki, nchini Finland.

No comments:

Post a Comment