SIMBA ya Dar
es Salaam ipo katika harakati za kuimarisha kikosi chake na sasa imefanikiwa
kumrejesha nyumbani kiungo wake Mwinyi Kazimoto.
Kazimoto
aliyekuwa akichezea klabu ya Al Markhiya ya Qatar, amerejea kwenye klabu hiyo
baada ya mkataba wake na klabu hiyo ya Qatar kumalizika.
“Tumemalizana
naye kijana, amesaini mkataba wa miaka miwili, naamini mambo yatakuwa sawa.
Dhamira yetu ni kuimarisha kikosi chetu,” kilisema chanzo cha kuaminika ndani
ya Simba.
Mtoa habari
huyo alieleza kuwa wanaamini kusajiliwa kwa Kazimoto kutaifanya Simba kuwa na
kikosi imara zaidi, ambacho kitarejesha hadhi ya klabu hiyo.
Hata hivyo
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alipoulizwa jana
kuhusiana na habari hizo alisema hafahamu lolote.
“Hapana
waone watu wa Kamati ya Usajili ya Simba, mimi sifahamu lolote ndugu yangu,”
alisema Manara.
Mapema mwezi
huu, Simba ilimrejesha mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi akitokea Mtibwa Sugar ya
Morogoro. Mgosi kama ilivyokuwa kwa Kazimoto naye aliwahi kuchezea Simba miaka
ya nyuma.
Kazimoto
aliyejiunga na Simba SC mwaka 2011 akitokea JKT Ruvu, aliuzwa mwaka 2013, Al Markhiya, ambayo ipo Ligi Daraja la
Pili nchini humo.
Wachezaji
wengine wa hapa nchini waliosajiliwa Simba hadi sasa licha ya Mgosi na Kazimoto
ni Peter Mwalyanzi kutoka Mbeya City, Mohamed Fakhi kutoka JKT Ruvu na Samih
Haji Nuhu kutoka Azam FC.
Pia Simba
imemsajili mshambuliaji wa Vital ‘O ya Burundi, Laudit Mavugo na mshambuliaji
wa zamani wa Yanga, Hamisi Kiiza.
No comments:
Post a Comment