Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 19, 2015

ZIG ZAG TANGA RALLY KUFANYIKA MEI 3

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Mehul Asher akizungumza ofisini kwake,Picha na Mpiga Picha Wetu.

MASHINDANO ya mbio za Magari ya “Zig Zag Tanga Rally 2015” yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi mkoani Tanga Mei 3 mwaka huu mzunguko wa pili kwenye yale ya Kitaifa chini ya ufadhili wa Zig Zag.
Mashindano hayo yatakuwa ya umbali wa km 135 na yatakuwa na awamu tano, yatakayoanzia katika hotel ya Tanga Beach Resort na kupitia maeneo ya Pongwe, Mkanyageni na Mjesani na kurudi yalipoanzia.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Mehul Asher alisema maandalizi yanaendelea vizuri na washiriki kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wamejiandikisha kushiriki
Alisema kuwa madereva watakaoshiriki katika michuano hiyo wanatazamiwa kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga ikiwemo wengine kutoka nchi za Kenya na Uganda.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mashindano hayo msimu huu yatakuwa na upinzani mkubwa kutokana na barabara watakazotumia washiriki ni nzuri hivyo itaweze kuwapa fursa kushindana vema.
Aidha alisema kuwa makabidhiano ya zawadi zilizoandaliwa kwa washindi mbalimbali zitafanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Dr. Fennela Mukangara

No comments:

Post a Comment