Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 12, 2015

MRWANDA WA YANGA KUIKOSA PLATINUM JUMAPILI



MSHAMBULIAJI Danny Mrwanda wa Yanga anazalimika kukosa mchezo wa dhidi ya Platinum ya Zambabwe utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza jijini Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro alisema kwamba, Mrwanda alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI nchini Botswana, hivyo hatacheza Jumapili.

“Mrwanda kwenye mchezo dhidi ya BDF XI nchini Botswana alionyeshwa kadi nyekundu hivyo atakuwa natumikia adhabu hiyo ndio maana hajaingia kambini”, alisema Muro

Yanga SC itamenyana na Platinum FC Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza, raundi ya kwanza ya Kombe la Shrikisho Afrika  hivyo Mrwanda atakuwa jukwaani.

Muro amesema Mrwanda amepewa ruhusa maalum ya kutokuwa kambini, ili akamsaidie mke wake kwa sababu amejifungua.

Awali kulikuwepo na tetesi kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC amesimamishwa kwa madai alicheza chini ya kiwango baada ya timu yake kufungwa na Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliochezwa jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.

Mrwanda alishindwa kuifungia Yanga bao la wazi dakika ya 28, baada ya kupewa pasi nzuri na Simon Msuva, lakini akazubaa na mpira ndani ya eneo la penati hadi akapokonywa na Juuko Murushid.

Tukio hilo lilimkera kocha Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm ambaye alimtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Javu

No comments:

Post a Comment