Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 25, 2015

RATIBA UEFA CHAMPIONS LEAGUE LEO: ARSENAL v AS MONACO, BAYER 04 LEVERKUSEN vs ATLETICO DE MADRID

LEO JUMATANO, Februari 25, Uwanja wa Emirates Jijini London utamkumbusha mbali Meneja wa Arsenal Arsene Wenger wakati watakapoikaribisha AS Monaco ya France kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
AS Monaco ni Timu ya pili ambayo Wenger alikuwa Meneja wake baada ya kuanza kazi hiyo Mwaka 1984 huko Klabu ya Nancy-Lorraine Mwaka 1984 na 1987 kuhamia AS Monaco ambako alikaa hadi 1994 na Mwaka uliofuatia kwenda huko Japan kwenye Klabu ya Nagoya Grampus Eight na kisha kuhamia Arsenal Mwaka 1996.
Wakati Arsenal ipo Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England nyuma ya Chelsea na Man City, AS Monaco hivi sasa inakamata Nafasi ya 4 huko Ligi 1 Nchini France ikiwa nyuma ya Olympique de Marseille, PSG na Olympique de Marseille.
AS Monaco na Arsenal hazijawahi kukutana lakini Monaco wana Historia nzuri dhidi ya Klabu za England baada ya Mwaka 1997 kuitoa Newcastle nje ya UEFA CUP na kutinga Nusu Fainali na 1998 kuitoa Man United toka UEFA CHAMPIONS LIGI kwenye Raundi kama hii.
Pia Mwaka 2004 walifika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI baada ya kuibwaga Chelsea kwenye Nusu Fainali.
Lakini safari hii AS Monaco wana uhaba mkubwa wa Magoli kufuatia kuwatema Wafungaji wao Radamel Falcao kwa kumpeleka kwa Mkopo Manchester United na kumuuza James Rodriguez kwa Real Madrid kitu kilichowafanya wafunge Mabao 25 katika Mechi 26.
Lakini AS Monaco wanae Straika wa zamani wa Manchester United Dimitar Berbatov, mwenye Miaka 34, ambae licha ya kufunga Bao 6 tu kwenye Ligi 1 katika Mechi 18, Kocha wa Klabu hiyo, Leonardo Jardim, amemtaja kuwa ni silaha kubwa kwao kutokana uzoefu na umahiri wake hasa kwenye Bigi Mechi.
Hata hivyo, AS Monaco inakutana na Arsenal ambayo kwa Miaka Minne iliyopita imekuwa ikikwama hatua hii hii ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa mara mbili kutolewa na Bayern Munich na mara moja moja na Barcelona and AC Milan.

Kila upande utawakosa Wachezaji kadhaa kutokana na maumivu kwa Arsenal kutokuwa na Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Mikel Arteta, Abou Diaby na Mathieu Debuchy na Monaco huenda wakamkosa Beki wao wa Kushoto Layvin Kurzawa na Winga Yannick Ferreira-Carrasco huku Jeremy Toulalan, Tiemou Bakayoko, Ricardo Carvalho na Andrea Raggi wakiwa nje kabisa.Mzee Wenger kwenye mazoezi na Vijana wake juu ya Mtanange wa Leo kati yao na Monaco inayocheza League 1Jembe jipya PaulistaAlex SanchezAlex na Theo W.Kwenye mazoeziSanchez kwenye furaha wakati wa mazoeziMonaco Mjiandaeee!!Wachezaji wa Arsenal wlipokuwa wanafanya mazoezi kwenye Uwanja wao wa mazoezi ColnelLeo kwenye Uefa ni sisi na nyie Monaco Emirates

No comments:

Post a Comment