Pambano hilo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini, linatarajiwa kuwa na ushindani mkali kwa vile kila timu inapania kushinda ili kuibuka na ubingwa.
Simba ilifuzu kucheza fainali baada ya kuichapa Polisi Zanzibar bao 1-0 wakati Mtibwa Sugar iliitoa JKU kwa njia ya penalti tano tano baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare.
Akizungumzia pambano hilo, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, alisema hana wasiwasi wa timu yake kutwaa ubingwa.
Kocha huyo kutoka Serbia alisema, timu yake ipo imara na hawana hofu na wapinzani wao kwa vile wana uhakika mkubwa wa kutwaa ubingwa.
Goran alisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri na wana ari kubwa ya kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ya kihistoria.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime,alisema dakika 90 za mchezo ndizo zitakazoamua bingwa wa michuano hiyo.
Mecky alisema kikosi chake kipo mara na kinatambua nini la kufanya katika mechi hiyo na kusisitiza kuwa, hana hofu na wapinzani wao.
No comments:
Post a Comment