Gareth
Bale amesema hataki kuona nyota mwenzake Cristiano Ronaldo akiondoka Real Madrid
kurudi Uingereza kwenye ligi ya Premier.
Licha
ya Ronaldo kuendelea kufunga mabao ikiwemo matatu wikendi jana dhidi ya
Athletic Bilbao yaliomfanya afikishe rekodi ya ‘hat-trick’ ya 22 katika La Liga
na kufikia rekodi ya ligi iliyowekwa na wachezaji wa zamani Telmo
Zarra na Alfredo Di Stefan.
Ronaldo
amekuwa katika uvumi wa kutaka kurudi katika timu yake ya zamani ya Manchester United msimu ujao wa kiangazi.
Hivi
majuzi, zilizuka tetesi kuwa Ronaldo anaweza kurudi katika timu yake ya zamani
ya United ua Manchester City na Bale ametangaza hataki nyota mwenzake arudi
kwenye ligi ya Premier.
Amedhihirisha
ni mchezaji wa kiwango cha kimataifa amekuwa anafunga mabao mengi.
Bila
shaka, hatutaki aondoke na ninataka asalie hapa Real Madrid,” Bale alisema.
No comments:
Post a Comment