Mchezaji
huyo wa zamani wa kikosi cha Ujerumani ni miongoni mwa watu 22 walioamua ni
wapi kinyang'anyiro hicho cha mwaka 2018 na 2022 kitafanyika katika kura
iliofanyika mnamo mwezi Disemba mwaka 2010.
Akizungumza
katika mkutano wa kuimarisha mchezo huo, mwaka 2014 ,Beckenbauer alikataa
kusema ni nani aliyempigia kura ,ijapokuwa ilidaiwa kuwa alipendelea fainali hizo zifanyike nchini Australia.
''Ilikuwa
ni kura ya siri,nilishangaa kuona Qatar ikiibuka mshindi'',Alisema mchezaji
huyo mkongwe.
Mchezaji
huyo wa zamani ambaye alishinda kombe la dunia kama mchezaji na meneja wa timu
ya Ujerumani ,aliongezea kuwa,ushindani ulikuwa mzuri,kama ile mingine lakini
hakukuwa na tofauti kubwa.
Lazima
kuna sababu kwa nini zile nchi nyengine hazikufanikiwa kuandaa fainali.
![]() |
Beckernbeur enzi za uchezaji wake |
Qatar
iliishinda Australia,Japan ,korea kusini na Marekani katika kura ya kuandaa fainali
za kombe la dunia mwaka 2022,huku Urusi
ikiishinda Uingereza pamoja na Ubelgiji na Uholanzi,Ureno na Uhispania kwa haki
ya kuandaa kombe la dunia la mwaka 2018.
Ni
kamati kuu ya FIFA ndiyo iliyotoa uamuzi huo ambao umekumbwa na utata tangu
tangazo hilo lifanywe.
Wanachama
wawili wa zamani wa Shirikisho hilo walizuiliwa kushiriki katika kura hiyo
kutokana na madai ya ufisadi,huku wengine sita wakilazimishwa kujiuzulu baada
ya kura hiyo.
Backenbauer
alijiondoa katika kamati hiyo mnamo mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment