Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, September 30, 2014

WAYNE ROONEY AIOMBA RADHI KWA KADI NYEKUNDU

Wayne Rooney amewaomba radhi Wachezaji wenzake kwa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi huko Old Trafford wakati Manchester United inaifunga West Ham. 

Rooney alipewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 54 na Refa Lee Mason kwa kumchezea Rafu Stewart Downing na amesema hana mpango wa kukata Rufaa. 
Kutokana na Kadi hiyo, Rooney atazikosa Mechi 3 za Ligi ambazo ni dhidi ya Everton, WBA na Chelsea na atarejea Uwanjani Novemba 2 kwenye Dabi ya Jiji la Manchester dhidi ya Man City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Kuhusu Kadi hiyo, Bosi wa Man United, Louis van Gaal, alikiri kuwa ilistahili kwani alikosea jinsi ya kumsimamisha Downing aliekuwa akichanja mbuga . 

Mwenyewe Rooney ameeleza: “Nilimwona Mchezaji wa West Ham akifanya kaunta ataki na mimi nilijaribu kuvunja hiyo lakini nilikosea namna ya kumzuia. Nimefarijika wenzangu walilinda Bao zetu na tumeshinda.”

No comments:

Post a Comment