Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, September 30, 2014

Ligi ya mabingwa Ulaya Manchester City kuivimbia Roma leo?

Baada ya masikitiko katika dakika za mwisho dhidi ya Bayern Munich wakati wa mechi yao ya kwanza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ngazi ya makundi, Manchester City hawawezi hawatakuwa tayari kuteleza tena watakapokutana na Roma kesho Jumanne uwanjani Etihad. 

Bao la dakika ya 90 la kijana wa zamani wa City Jerome Boateng liliwatunuku Bayern ushindi wiki mbili zilizopita, na baada ya Roma kuanza kampeni yao Kundi E kwa kuiponda CSKA Moscow 5-1, mabingwa hao wa Uingereza tayari wanakabiliwa na presha kiasi. 

Baada ya kurarua Sheffield Wednesday 7-0 katika League Cup kabla ya kulaza Hull City 4-2 ligini Jumamosi, vijana hao wa Manuel Pellegrini wanafunga mabao mengi, lakini mkabaji wa kulia Pablo Zabaleta anajua Roma watakuwa tofauti. 

“Sasa tunahitaji kufungua ukurasa mwingine na kufikiria tu kuhusu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya,” beki huyo wa kulia wa Argentina aliambia televisheni ya City baada ya ushindi dhidi ya Hull. 

“Tulipoteza mechi dhidi ya Bayern Munich na sasa tutakabiliana na Roma nyumbani. Tunajua umuhimu wa kushinda mechi hiyo. 

“Itakuwa mechi nyingine ngumu kwa sababu Roma pia ni wazuri, tunatumai tutacheza vyema na kupata alama tatu.”
Kihistoria, Roma hawajakuwa na matokeo mema dhidi ya klabu za Uingereza.

Walishindwa kupitia mikwaju ya penati na Liverpool mara yao pekee kucheza fainali ya ubingwa Ulaya 1984 na wameshinda moja peke kati ya 14 walizocheza Uingereza. 

Manchester ulikuwa pia mji waliopokezwa mojawapo ya vichapo vikubwa zaidi walipolazwa 7-1 na wapinzani wa City jijini Manchester United kwenye robo fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2007. 

Lakini ingawa City hawajawahi kulazwa na klabu ya italia katika mechi nne za majuzi, zaidi watatahadhari sana dhidi ya timu hiyo ambayo sasa inapigania ubabe wa Serie A na Juventus.
Vijana hao wa Rudi Garcia wameshinda mechi zao zote sita walizocheza katika ligi msimu huu, ikiwa ni pamoja na ushindi wa 2-0 dhidi ya Hellas Verona uliowaweka sawa kwa alama na Juventus kileleni kabla ya kivumbi kati ya timu hizo mbili mjini Turin wikendi hii. 

Ushindi wa Jumamosi dhidi ya Verona ulifanya Garcia kufikia alama 100 Serie A katika mechi yake ya 43 kileleni – mapema kushinda kocha mwingine yoyote wa awali Roma – na anasema klabu yake itazuru Manchester ikiwa bila wasiwasi. 

"Itakuwa mechi kubwa. Hawana alama, hivyo ndio walio na presha. Wanahitaji matokeo kwao nyumbani,” alisema Mfaransa huyo, ambaye vijana wake walimaliza wa pili nyuma ya Juve nchini Italia msimu uliopita. 

"Tuko thabiti na tumeonyesha kuwa na imani kubwa katika uchezaji wetu.

Tuko tayari kukabili changamoto zinapochipuka, lakini lazima tufurahie mechi hii na kubeba kile tutakachofanikiwa.”

No comments:

Post a Comment