TIMU ya Azam FC leo imefungwa mabao 2-1 AS FAR Rabat kwenye
mchezo wa kombe la Shirikisho barani mchezo uliochezwa Uwanja wa Prince Moulay
Abdellah nchini Morocco
Azam ilihitaji sare yoyote ya mabao ili iweze kufuzu lakini
dakika ya 81 ilipata penalti ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, lakini fundi wa upigaji
wa michomo hiyo, John Raphael Bocco alikwenda kugongesha mwamba mpira huo na
kurudi uwanjani.
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita,
mfungaji John Raphael Bocco kwa mpira wa adhabu, baada ya beki mmoja wa AS FAR Rabat
kushika mpira kwenye eneo la hatari.
Iliwachukua dakika sita tu AS FAR Rabat kusawazisha kupitia
kwa Abdelrahim Achchakir kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki David Mwantika
kumchezea rafu mchezaji wa AS FAR Rabat.
Abdelrahim Achchakir alitolewa nje kwa kuonyeshwa kadi
nyekundu baada ya kumchezea rafu Brian Umony dakika ya 35 lakini SA FAR Rabat
wakiwa pungufu waliongeza bao la pili kupitia kwa Mustafa Allaoui alipiga
vizuri shuti la mpira wa adhabu dakika ya 42.
Kipindi cha pili, mchezo ulizidi kuwa wa kasi na kushambuliana kwa zamu na dakika ya 56 beki wa
Azam David Mwantika kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu
mchezaji wa AS FAR Rabat. Na Waziri Salum alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya
75 baada ya kumchezea rafu Kaddioiu Yuossef.
Pamoja na Azam kuwa pungufu waliendelea kulishambulia lango
la AS FAR Rabat na dakika ya 81 beki wa AS FAR Rabat alishika mpira kwenye eneo
la hatari na mwamuzi akamuru penalti ambayo Bocco alikosa baada ya shuti lake
kugonga mwamba.
Azam imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya mchezo wa awali
wiki mbili zilizopita kutoka sare ya bila kufungana Dar es Salaam na Waarabu
hao.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri
Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum
Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Gaudence Mwaikimba dk79 na Brian Umony/Khamis Mcha dk70.
AS FAR Rabat; Ali Grouni, Anouar Younes/Ennajar Tarik,
Younes Hammal, Younes Belakhdar, Kaddoui Youssef, Abdelrahim Achchakir, Aqqal
Salaheddine/Alloudi Soufiane, Mustafa Allaoui, El Kodry Yassine, El Bakkali
Medamine na El Yousfi Mostafa.
No comments:
Post a Comment