Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 8, 2013

WAHARIRI NA WAANDISHI WAANDAMIZI KUKUTANA ARUSHA APRILI MWAKA HUU

SEMINA na kikao cha wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa michezo na burudani  nchini, vinatarajiwa kufanyika April 12 na 13  mwaka huu, katika jiji la  Arusha.
Semina hiyo, pia itakwenda sambamba na kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine ambapo wanahabari hao watatembelea familia na Kaburi la  Sokoine wilayani Monduli ili kutoa pole.
Maamuzi ya kufanyika semina hiyo na kikao cha wahariri jijini hapa, yalifikiwa juzi katika kikao baina ya Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari zamichezo  nchini(TASWA), Juma Pinto na viongozi wa TASWA Arusha katika hoteli ya palace  mjini hapa. 

Akizungumza katika kikao hicho, Pinto alisema TASWA inatarajia kuitisha kikao hicho, Arusha ikiwa ni sehemu ya mipango yake,kukifanya chama hicho kuwa  cha kitaifa zaidi na pia kuongeza uelewa  wa masuala ya michezo kwa wanahabari.  

“kamati ya utendaji ya TASWA taifa hivi karibuni ilikutana ambapo pamoja na mambo mengine iliamua kuifanya kikao na  semina ya wahariri mkoani Arusha hivyo nimekuja hapa ili tushauriane kuwezesha semina na kikao hiki”alisema Pinto.

Pinto  alisema ili kufanikisha semina hiyo, TASWA taifa na Taswa Arusha, wanapaswa kushirikiana katika maandalizi ya kutafuta wadhamini, ambapo  pia watashirikishwa wanahabari toka mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Manyara.  

Wakizungumza katika kikao hicho,  Katibu wa  TASWA Arusha, Mussa Juma na Katibu msaidizi Hamza Kalmera walieleza TASWA Arusha kuwa tayari kuandaa  semina hiyo, ambayo itafanyika siku ya kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri mkuu, Edward Moringe Sokoine pia  kutafanyika tamasha maalum la michezo  mbali mbali.

Juma alisema  TASWA Arusha  itajipanga kuhakikisha wakati wa semina hiyo, wahariri na waandishi wa habari waandamizi watapata fursa ya kutembelea kaburi la Sokoine  wilayani Monduli kama ishara ya kumuenzi.
"tutajipanga wanahabari waende Monduli juu kutoa pole kwa familia ya Sokoine na  pia siku ya April 13 kufanyike mchezo kati ya TASWA Arusha na TASWA Dar es salaam"alisema Juma.
Katika semina hiyo, pia wanahabari hao, wanatarajiwa kupata taarifa ya awali ya marekebisho ya katiba  ya TASWA na pia taarifa ya uanzishwaji wa chama cha kuweka na kukopa  TASWA SACCOs.

No comments:

Post a Comment