Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 8, 2013

LADY JAY DEE AANZA SAFARI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

MSANII mkongwe katika Tasnia ya muziki hapa nchini, Judith Wambura maarufu Lady Jay Dee, jana alianza safari ya siku sita ya kupanda Mlima Kilimanjaro. 

Lady Jay Dee akiwa ameongozana na Meneja wake ambaye pia ndiye Mume wake, Gardner Habash, anatarajia kutumia siku sita kupanda mlima huo mrefu zaidi barani afrika.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO kwa njia ya simu akiwa katika kilele cha uhuru kilichoko zaidi ya mita 5859, alisema kuwa lengo la kupanda Mlima Kilimanjaro, ukiacha programu yake ya kuandaa kipindi chake kinachorushwa na EATV kila siku ya jumapili kiitwacho Diary ya Lady Jay Dee, anatarajia kutumia nafasi kuhamasisha Watanzania kuupigia kura Mlima huo kuingia katika Maajabu Saba ya Dunia.

“Lengo langu ukiacha lile la kupiga picha za Diary yangu inayorushwa EATV, nataka kutumia uwezo wangu na ushawishi wangu kama msanii kuhamasisha kupanda mlima Kilimanjaro na inatakiwa kila Mtanzania kuthamini, kulinda na kujivunia urithi huu,” alisema Jay Dee.

Jay Dee alisema kuwa, Watanzania wanatakiwa kujiwekea utaratibu wa kupanda na Kuenzi Mlima Kilimanjaro kila mara  na kuongeza kuwa Mlima Kilimanjaro, ambao ni Mlima mrefu zaidi barani Afrika ni mali na urithi wa kila mtanzania hivyo ni vizuri kila mtanzania kujivunia raslimali tulizonazo kwa kuzitembelea na sio kuwaachia wazungu pekee.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wasanii kutumia nafasi waliyonayo kupanda Mlima, kuhamasisha upandaji wa Mlima, na sio kuacha shughuli hiyo kwa Wageni kutoka nje kuja kututangazia Mlima wetu na kuongeza kuwa ni vyema kila Msanii kujikita mambo yenye tija na Taifa.

Kwa upande wake, Gasto Mosha ambaye ndiye anayemuongoza Msanii huyo katika safari yake ya upandaji Mlima, alisema atahakikisha Msanii huyo anafika kileleni ili aweze kuutangaza vyema Mlima  kwa Wasanii kumuunga mkono Lady Jay Dee.





 Lady JayDee(katikati) Deogratias (kulia) and Gasto Mosha (kushoto) atakayemuongoza Msanii huyo hadi kilele cha Uhuru -Peak 5895m


 Lady Jaydee akiwa na mpiga picha wake Justin Bayo katika Geti la Marangu 





Lady Jaydee na Gardner Habash baada ya kusaini daftari la Wageni katika Geti la Marangu leo


 Lady Jaydee katika pozi kabla ya kuanza kupanda Mlima


 Lady Jaydee akitia sahihi katika Daftari la Wageni


  kundi la wapandaji kabla ya kupanda Mlima

 Mhifadhi Mkuu wa Mlima Kilimanjaro, Erastus Lufungilo akisalimiana na Lady Jaydee kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro zoezi litakalochukua siku sita.


  Picha ya Pamoja na wapandaji wengin,(kutoka kushoto)  Deogratias (guide), Justin Bayo(mpiga picha) Gardner G Habash Mume Wake), Gastor Mosha(guide) Lady Jay Dee, George(Kilidove Tours) Emanuel(porter) and Mr Erastus Lufungilo (Mhifadhi Mkuu)



Lady Jaydee katika Ofisi ya Mhifadhi Mkuu kabla ya Kupanda Mlima Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment